Wednesday , 16th Jul , 2014

Mwanamuziki maarufu wa Reggae barani Afrika Jhikoman anatarajia kupanda jukwaani wiki hii katika maonesho ya 5th International African Festival 2014 yatakayofanyika katika mji wa Tubingen, Ujerumani.

Mwanamuziki Jhikoman kutoka Tanzania

Mwanamuziki huyo kutoka nchini Tanzania ambaye yupo katika ziara ya kikazi barani Ulaya amepata pia kualikwa na kutembelea miradi mbalimbali ya utamaduni nchini Ujerumani zikiwemo shule na taasisi za muziki nchini humo.

Aidha, mkali huyo wa kibao maarufu cha 'Moyo Unadunda' amesema kuwa hivi sasa anatarajia kufanya kazi mbalimbali na vikundi vya muziki na amekuwa akifanya pia mazoezi ya viungo nchini Ujerumani.