Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Juliana Shonza ni zaidi ya mama yangu - Gigy Money

Monday , 24th Sep , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo na 'video vixen', Gift Stanford 'Gigy Money' amesema kitendo cha kuonywa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ni cha kishujaa kwa madai hata mama yake mzazi hakuweza hata siku moja kumuonya juu ya maisha yake anayoishi

Gigy Money akiwa na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza.

Gigy Money amebainisha hayo alipokuwa anaongea na www.eatv.tv mapema hii leo Septemba 24, 2018 na kusema kwamba siku zote mtu anayemtakia mema mwenzake ni lazima amwambie ukweli katika yale anayoyafanya nasio kuachwa apoteze muelekeo zaidi.

"Nimezipata taarifa za Naibu Waziri Juliana Shonza na nimeanza kuzifanyia kazi. Sioni kama amekosea kuniambia hivyo kwasababu yeye ni mkubwa na inawezekana hanitaki mabaya yanitokea katika maisha yangu kama wengine wanavyodhani au kufikiria, nahisi kuna vitu anaviona vizuri kutoka kwangu kwa kesho na kesho kutwa", amesema Gigy Money.

Pamoja na hayo, Gigy Money ameendela kwa kusema kuwa "nahisi Shonza ana mapenzi ya dhati na mimi, maana hii mara ya pili ananipa 'chance' ya kubadilika, siku zote anayekwambia ukweli anakupenda. Kiukweli nime 'appreciate' kwasababu hata mama yangu mzazi hawezi kuniambia alichoniambia yeye".

Aidha, Gigy Money amesema kwamba sio jambo rahisi kwa yeye kuzifuta picha zake zilizokuwa zinamuonyesha amevalia mavazi ya nusu utupu, kwa madai picha hizo zina kumbukumbu kubwa katika maisha yake pamoja na sehemu alizozipigia wakati huo.

"Kufuta picha hakumaanishi mtu kwamba amebadilika bali kubadilika ni mtu mwenyewe kufanya hicho kitendo kutoka moyoni kabisa, halafu picha zangu hazihusiani na maisha yangu halisi. Instagram mimi ndio inanilisha na kuniweka mjini kwa kila jambo", amesisitiza Gigy Money.

Kauli hizo za Gigy Money zimekuja baada ya kupita chache tokea Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kumpa onyo la mwisho msanii huyo kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii na endapo hatofanya hivyo basi atamchukulia sheria stahiki dhidi yake.

Msikilize hapa chini Gigy Money akielezea zaidi.....

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya