Sunday , 27th Aug , 2017

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi baada ya kusikiliza wimbo mpya wa msanii wa bongo fleva King Kibaa 'Alikiba',  ameahidi kumpatia zawadi msanii huyo kwa kile alichodai kazi imekwenda shule.

Alikiba

Mhe. Hapi ameshindwa kuzuia hisia zake juu ya Alikiba ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii huyo aachie ngoma mpya aliyoipa jina la 'Seduce me' ikiwa ni baada ya kukaa mwaka 1 na miezi kadhaa tangu alipotoa wimbo wake wa Aje ukiachana na Remix ya wimbo huo alioutoa miezi sita iliyopita.

Kupitia ukurasa wake Instagram Mhe. Hapi ameandika ”Nimekuelewa sanaa wajina @officialalikiba. Kazi imeenda shule. Nidai zawadi kwa muziki huu wa ukweli. Keep the fire burning! #seduceme.” 

Hata hivyo wimbo huo umeonekana kukonga nyoyo za wasanii mastaa mbalimbali akiwepo muigizaji Wema Sepetu ambaye kwa upande wake amedai umemuathiri.

"I have something to tell Alikiba... Baba Tunashukuru kwa muziki mzuri, unatukomesha sana... Unatupa shida masaa yote nyimbo inakuwa kwenye repeat... Yaani sijioni naskiza nyimbo nyingine zaidi ya #SeduceMe ..