
Nandy
Nandy alisema hayo kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV na kusema anapokea sana request za mashabiki zake wakihitaji video lakini alishindwa kufanya kwa wakati sababu alilazwa kwa matatizo ya vidonda vya tumbo.
"Unajua wimbo wangu wa One day umetoka kama wiki kadhaa hivyo nimekuwa napokea request nyingi kutoka kwa mashabiki wakitaka video, lakini tumshukuru Mungu hata leo nipo hapa maana kama wiki moja hivi nilikuwa siwezi kuamka hata kitandani nilikuwa nasumbuliwa na 'Stomach ulcers' hivyo nilishindwa kufanya hata vitu vyangu binafsi ili nawaahidi kuanzia sasa muda wowote video ya One day itatoka" alisema Nandy