Tuesday , 19th Aug , 2014

Rapa Kitifa kupitia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la "Unacheza na Nani" ft Rich Mavocal, amesema kuwa kazi hiyo imeweza kuzishika chati mbalimbali kutokana na muunganiko mzuri wa wasanii pamoja na timu ya watayarishaji.

msanii wa muziki nchini Kitifa

Kitifa amesema kuwa, baada ya kazi hii kufanya poa katika upande wa Audio, sasa anarudi tena na video yake ya pili kubwa ikifuatia ile ya ngoma ya Maisha ya Mjini ambayo alishirikiana poa na msanii Linex Mjeda.

Video ya kazi hii itatoka rasmi Jumatatu tarehe 25 mwezi August.