
Abbas ametaja mambo muhimu ambayo mamlaka hii inatakiwa kushughulikia kurekebisha, ikiwepo wasanii kuitwa katika vikao katika hatua za mwisho, njia za kuwasiliana na wasanii kuimarishwa, na pia kutokupendelea lebo moja dhidi ya nyingine kati ya mambo mengine.
Abbas kutokana na malalamiko haya, ameandaa waraka ambao atatumia kukusanya saini za wadau na wasanii watakaomuunga mkono ili kuwezesha kusukuma mambo haya ya msingi kushughulikiwa na kuwekwa katika mstari.