
Msanii wa Bongo Fleva, Linah na mpenzi wake, Shaban mchomvu
Linah amefunguka hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv, alipoulizwa
juu ya habari inayoendelea katika mitandao ya kijamii ikisemekana kuwa amemwagwa na baba watoto wake, Shaban mchomvu, ambaye ni mfanyabiashara na msimamizi wa wasanii.
''Sidhani kama mashabiki wangu wanatakiwa kufahamu kuhusu maisha yangu binafsi, wanachopaswa kukifahamu ni mziki wangu tuu, kwa hiyo siwezi kuzungumzia swala hilo,'' amesema.
Linah ameongeza kuwa anatarajia kutoa wimbo mpya siku yoyote kuanzia sasa, hivyo wapenzi wa muziki wasubiri ujio wake mpya.
''Nitaachia wimbo mpya hivi karibu ambao una video tayari, kwa hiyo
mashabaki wangu watengeme kupata kitu kizuri kuanzia sasa,'' ameongeza
Linah.