Saturday , 29th Apr , 2017

Msanii mchanga anayekuja kwa kasi kupitia hit yake ya 'Sina Koloni' aliyomshirikisha G Nako, Motra the Future amefunguka na kuweka wazi kwenye story tatu ya Planet Bongo kuhitaji mafanikio ya haraka ndiyo chanzo cha kuondoka kwa Mona Gangsta.

Motra the Future

Motra amefunguka hayo baada ya kuwepo maneno ya kwamba alikuwa aking'ang'ania kutaka kujulikana kabla hajaiva chini ya upishi wa Producer na mmiliki wa Classic Sound Music, Mona Gangstar ambaye pia alikuwa meneja wake kitu ambacho Motra amekipinga vikali na kuamua kulitolea ufafanuzi.

"Mimi ni kijana ambaye nahitaji mafanikio ya haraka kwa hiyo niliondoka kwa Mona kwanza ili nikajitafutie hayo mafanikio niliyokuwa nayataka. Kwa Mona Gangstar sijaondoka kwa ubaya na ninauhakika nikifanikisha ninayoyawaza nitarudi tena kwake ili tufanye sasa kazi" Motra The Future alifafanua.

Aidha Motra amemtaka Producer huyo kujipanga vizuri kabla ya kuanza kumiliki wasanii ili kuepuka matatizo ya kutoelewana na wasanii anaowasaini.
"Lakini mimi namshauri Mona kabla hajaamua kusimamia wasanii. Yale yote ambayo ameyaahidi kwenye mkataba ahakikishe anayakamilisha. Kama msanii...mimi natakiwa niwe na muonekano wa kisanii na siyo tena napita mtaani watu wanaanza kunyoosha vidole huyu si ndo kaimba video fulani haipendezi anatakaiwa ajue jinsi ya kuwatengeza wasanii hivyo lazima ajipange zaidi."- aliongeza Motra The Future