Thursday , 11th Aug , 2016

Baada ya shindano la Dance100% kumaliza raundi ya michuano ya usaili wa kwanza hadi wa tatu na kupatikana kwa makundi ya kushiriki hatua ya robo fainali, majaji wa mpambano huo wamegawana makundi ili kuweza kuwafundisha mbinu za kushinda shindano.

Majaji wa Dance100

Akizungumza na EATV Mratibu wa shindano hilo Bi. Bhoke Egna amesema majaji wa shindano wamegawana makundi kwa ajili ya kuwapa mbinu za kuweza kufanya vizuri kwenye shindano ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda pamoja na nidhamu.

''Makundi yote yaliyopita yamechagua majaji wa kuyafundisha ambapo mafunzo hayo yanaendelea na robo fainali itafanyika siku ya Jumamosi tarehe 13.08.2016 katika viwanja vya Oysterbay Jijini Dar es salaam'' Amesema Bhoke.

Aidha kwa upande wake Jaji wa shindano hilo Super Nyamwela amewataka washiriki hao kuhakikisha wanafika kwenye maeneo waliyokubaliana kwa wakati na kuzingatia yote wanayoelekezwa ili kuweza kutambulika kwa jamii na hatimaye kujishindia kitita cha milioni 7 ambapo ni udhamini maridhawa wa Vodacom na Coca-Cola na kuonekana na EATV kila Jumapili saa moja jioni.

Makundi hayo yamechagua majaji wa kuwafundisha kama ifuatavyo.

Kundi - Jaji
Tatanisha Crew -Nyamwela
B.B.K Crew Boys -Khalila
Mazebe Powder - Lotus
D.D.I Crew - Lotus
The Quest Crew - Khalila
The Hero's Crew - Khalila
Clevers Boys - Nyamwela
Mafia Crew - Khalila
T.W.C Crew - Lotus
Makorokocho - Nyamwela
Ikulu Vegas Crew - Nyamwela
Wazawa Crew - Lotus
J Combat Crew - Lotus

Tags: