Saturday , 13th Aug , 2016

Shindano la Dance100% limemaliza vyema hatua ya robo fainali ambayo imefanyika katika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki huku zawadi mbalimbali kutoka Vodacom na Coca-Cola zikitolewa kwa mashabiki

Kundi la Wazawa Crew lilipokuwa likishiriki hatua ya robo fainali.

Makundi ambayo yameweza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya mchuano mkali wa kuonesha ufundi wa kucheza ni haya yafuatayo:

1. Wazawa Crew
2. D.D.I Crew
3. Team Makorokocho
4. J Combat
5. Clever Boys
6 B.B.K Boys
7. The Quest Crew
8. Tatanisha Crew
9. The Heroes
10. Mazabe Powder

Makundi yaliyoaga shindano ni pamoja na Mafia Crew, TWC pamoja Ikulu Vegas.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa washindi hao Jaji Lotus amewataka kuendelea na mazoezi kwani hatua ya nusu fainali, makundi matano yataaga mashindano ili yabakie matano yatakayopambana kwa ajili ya hatua ya fainali.

Kwa upande wake Jaji Khalila amesema makundi ya leo yameweza kuonesha ufundi wa hali ya juu ambapo kama yakiendelea hivyo yataweza kufanya vizuri katika shindano na hata nje ya shindano la Dance100%.

Aidha kuweza kuona tukio zima la Dance100% fuatilia EATV kila siku ya Jumapili saa moja kamili jioni ambapo hatua zote zitaoneshwa kuanzia usaili hadi hatua iliyofikia sasa.

Tags: