Friday , 12th Aug , 2016

Robo fainali ya Dance100% inafanyika kesho katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Dar es salaam kuanzia saa sita mchana na kuendelea ambapo makundi 13 kupambana na matatu yataaga mashindano hayo ambapo 10 yatabakia ili kuchuana nusu fainali.

Kundi la Mafia Crew

Akizungumzia mchuano wa kesho mmoja wa waratibu wa shindano hilo Brendansia Kileo amesema maandalizi ya siku ya kesho yapo vizuri hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna vijana walivyojipanga kuonesha vipaji.

“Kesho makundi matatu yataaga mashindano kwa kuwa lengo letu ni lazima mshindi apatikane, hivyo majaji wetu watakuwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha kwamba wanaotimiza vigezo sawasawa wanabakia katika shindano, pia kutakuwa na zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamini wetu Vodacom na Coca-Cola hivyo si siku ya kukosa”-Amesema Kileo.

Aidha shindano la Dance100% linaonyeshwa kila siku ya Jumapili saa moja jioni kupitia EATV pekee, ambapo makundi yote yataoneshwa namna yalivyochuana kusaka nafasi ya kuendelea na shindano.

Tags: