Tuesday , 26th Aug , 2014

Msanii anayefanya muziki wake wa kiasili na kiafrika zaidi aliyeweza tamba na kichupa chake maarufu kilichobatizwa jina 'Akateka', Man Kassu arudi na ujio mpya alioubatiza jina Man Kassu The Power, Man Kassu The Imaginator.

msanii wa muziki wa asili nchini Man Kassu

Man Kassu ambaye hivi sasa alikuwa kimya akifanya kazi zake za utafiti katika mikoa kadhaa nchini ameielezea eNewz kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayoitwa 'Goma' chini ya Man Water wa Combination Sound.

Amesema kuwa wimbo huo wenye mahadhi ya kiswahili utafanyiwa shooting katika mikoa mitatu ikiwemo Mwanza, Manyara na kumalizia Jijini Dar es Salaam ndani ya mwaka huu.

Aidha, mkali huyo ambaye yu mbioni kusaini mkataba na kampuni ya Masamaki Ent. ameonesha kuwazimia wasanii nyota wakiwemo Jide, Linah, na 20% hii ni kutokana na aina yamuziki wanaoufanya na ndoto zake za usoni ni kufanya nao kazi.