Friday , 16th Nov , 2018

Msanii wa mziki wa kizazi kipya mwenye sauti yenye mvuto wa kipekee, Ruby, amekalishwa kitimoto kwenye mitandao ya kijamii na mtanzania Mange Kimambi, akionywa ili aache tabia yake ambayo wengi wamekuwa wakilalamikia.

Mange Kimambi aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram akimtaka aache kiburi, ili aweze kufika mbali zaidi, kwani kwa upande wa kipaji msanii huyo amejaliwa kipaji kikubwa kuliko wasanii wengi wa kike hapa bongo.

“Ruby mdogo wangu 'you are super talented' ila ushauri punguza jeuri kidogo basi, maana naambiwa we ni mkorofi hata dada yako sikufiki kwa ukorofi na ujeuri.....Acha basi basi mdogo wangu maana talent yako ni kubwa mno, ulipo sasa ni chini sana compared na talent yako.”, ameamdika Mange Kimambi.

Mange Kimambi aliendelea kumuweka sawa msanii huyo huku akimtolea mfano mwanamuziki nguli bongo Lady Jaydee.

Baada ya jumbe huo Lady Jaydee na Vanessa Mdee waliingilia kati na kutia neno, wakimuonya msanii huyo ambaye wengi wamekuwa wakimlalamikia kuwa na kiburi na dharau.