Saturday , 20th Sep , 2014

Mtayarishaji muziki anayefanya vizuri katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya Tanzania, Mr T Touchez amezungumzia suala zima la dharau kwa baadhi ya wasanii katika gemu ya muziki na kusema kuwa tabia hii ipo sana ingawa kwa yeye binafsi haimuathiri.

Ney Wa Mitego na Mr T Touchez

Mr T Touchez ambaye sasa anafanya kazi chini ya Studio mpya za Freenation amesema kuwa, tabia hii ya dharau si tu kwa 'industry' ya muziki, bali hata nje ya sanaa hiyo, na kwa sehemu kubwa ni tabia ya ndani ya mtu ambayo haisababishwi na sanaa, isipokuwa malezi.

Tags: