
Young Thug
Rapa huyo ametangaza uamuzi wake baada kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, ambapo amesema,"nina nia ya kugombea Urais 2024, Gunna atakuwa makamu wangu wa Rais".
Aidha rapa huyo amewahi kuzua kituko kwa kutangaza kujiita jina la 'Sex', kutokana na kupendelea kuvaa nguo za kike.
Msanii mwingine aliewahi kutangaza nia ya kuwa raisi ni rapa Kanye West, kutokana na kuwa karibu na Rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump.