Saturday , 21st Jun , 2014

Shindano kubwa kabisa la Nice and Lovely Miss Tanga 2014, linatarajiwa kuwa kivutio kikubwa siku ya leo Jijini Tanga pale Mkonge Hotel, katika tukio ambalo litabarikiwa na ugeni mzito kabisa wa Mkuu wa Mkoa, Luteni mstaafu Chiku Gallawa.

Washiriki wa Nice and Lovely Miss Tanga 2014 katika picha ya pamoja

Warembo 14 akiwepo Zuhura Masoud, Irene Hermes, Diana Festo, Fatma Iddy, Faith Joel, Elvira Arbogast, Abigael Mathias, Yusta Philip, Nasra Ramadhan, Upendo lyimo, Degy Wilfred, Janeth Maimu na Pendo Ayoub watachuana vikali kuonesha uwezo wa kushikilia taji hilo.

Mshindi atakayepatikana leo atachomoka na zawadi nono ya gari aina ya Vitz, huku mshindi wa pili akikabidhiwa kitita cha shilingi laki 5, laki 2 na nusu kwa mshindi wa tatu, na laki 1 kwa mshindi wa nne, na vile vile wale watakaoshindwa watapatiwa kifutajasho cha shilingi 50 kila mmoja.

Tiketi za onyesho hili zinapatikana kwa shilingi 10,000 tu kwa viti vya kawaida, na 30,000 kwa VIP, Burudani kali kutoka kwa malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa atakuwepo ili kutia nakshi za burudani za Pwani katika mashindano haya.