.jpg?itok=gTfbQ3SH×tamp=1473568348)
Dudu baya ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa wengi wao hutumia kazi hiyo kutafuta umaarufu na kupata watu ambao watawawezesha kiuchumi.
“Wasiingie kwenye kuonekana au kuuza sura ili wajulikane then iwe rahisi kupata soko kwa sababu lengo lao ni michepuko, kwa hiyo anapokuwa anajulikana basi ni rahisi kuwapata mapedeshee ni rahisi kufanya michepuko yake, ni sawa sawa na kwenye bongo movie”, alisema Dudu Baya.
Dudu baya aliendelea kusema haya kuhusu mabinti hao.....“binti anapokuwa star anahitaji avae very expensive aendane na ustar wake, kwenye movie hapati hicho kipato, kwa hiyo anachokifanya ili apate mahitaji anataka gari kali, anataka nguo kali ang'ae kila wakati mwingine anataka kuanzisha kipindi chake cha TV aonekane naye ana kipindi, awe na duka lake kwa hiyo hivyo vyote anavipata kutoka kwa wanaume”.
Pia msanii huyo amewataka mabinti hao kutotumia uzuri wao kufanya kinyume na mapenzi ya Mungu, kwani si jambo zuri.
“Ni kujiheshimu na kujitambua kuwa uzuri ulionao umepewa na Mwenyezi Mungu hujapewa na shetani, endapo we ule uzuri unakurubuni na kuwa mtu wa michepuko basi unamdhalilisha mwenyezi Mungu na kumtukuza shetani”, alisema Dudu Baya.