
Miss Tanzania 2016 Dianaflave
Diana amefunguka kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio alipokuwa akipiga stori na Big Chawa, ambapo amesisitiza kuwa kutokana na gharama za maisha, Miss lazima awe na mwanaume wa kutoka naye mwenye pesa.
''Pesa anazo, ni muhimu, unadhani tutaishi vipi mtaani akiwa hana hela ? Pamoja na upendo lakini lazima miamala iwepo, tazama Miss Tanzania wote kama wanatoka na mtu ambaye hana pesa'', alifunguka.
Hata hivyo Diana aligoma kumtaja mpenzi wake akisema hayo ni maisha yake binafasi hapendi kuyaweka wazi kwa watu.
Kuhusu kulalamikiwa kutompa 'Support' Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth ambaye yupo nchini China kushiriki mashindano ya ulimbwende ya dunia, Diana amesema anafanya hivyo kimyakimya.
''Ni suala la kumpigia kura na kumwombea na nina fanya hivyo tatizo watu wanataka wakuone unaposti mtandaoni ndio wajue unamsapoti'', alimaliza.