Wednesday , 12th Nov , 2014

Msanii wa muziki Nameless amekanusha uvumi kuwa yeye na mkewe Wahu wapo katika mchakato wa kupeana talaka, sababu ikielezwa kuwa ni Nameless kugundua kuwa yeye si baba halisi wa mtoto wao Nyakio.

msanii Nameless wa nchini Kenya akiwa na mkewe Wahu

Nameless amesema kuwa, tetesi hizi zimeibuliwa mtandaoni na wahuni waliokuwa na lengo la kuvutia wasomaji katika kurasa zao, na kuwatoa hofu mashabiki wao kuwa yeye na mkewe na watoto wao wapo sawa kabisa.

Nameless ameongeza kuwa, tetesi za namna hii zinazoshambulia mahusiano yao zimeweza kuwafanya kuwa imara zaidi.