Monday , 22nd Feb , 2016

Staa wa muziki wa R&B Ne-Yo amefunga ndoa na mchumba wake mwanamitindo Crystal Renay katika tukio lililofanyika kwenye mgahawa wa Terranea ulioko Rancho Palos Verdes, California Jumamosi ya Feb 20 2016.

NE-YO NA CRYSTAL RENAY

Neyo ameliambia jarida la PEOPLE “Nina shauku kubwa ya kuwa pamoja na kuishi maisha yetu pamoja, tutakuwa kama kawaida, zaidi ya marafiki”.

Renay ana ujauzito wa Ne-Yo wa miezi tisa sasa na huyu ni mtoto wa tatu wa Neyo.

Neyo ana mtoto wa kike wa miaka mitano 'Madilyn Grace' na mvulana wa miaka minne 'Mason Evan' kutoka kwenye mahusiano yake na Monyetta Shaw.

Tags: