Sunday , 16th Mar , 2014

Baada ya msanii wa kike wa Jamaica Nyanda kuanza kushika chati na kuwa gumzo kupitia majarida na vituo mbalimbali vya muziki, msanii huyo anayefanya muziki wake akiwa sasa solo ameweka wazi kuwa haimaanishi kwamba amemtema dada yake Naila.

Nyanda na Naila wanaoliunda kundi moja la Brick and Lace amesema kuwa yeye na dada yake Naila wapo pamoja japokuwa Nail ameelekeza nguvu zake nyingi katika kazi za ubunifu wa ndani (interior design) wakati yeye Nyanda ameamua kufanya zaidi muziki.

Nyanda amesema kuwa hivi sasa wawili hao wamelamba mkataba na kampuni moja inayojishugulisha na usambazaji wa kazi za wasanii nchini Kenya itakayokuwa ikiwatangaza wasanii hao kupitia mitandaoni, na simu za mikononi barani Afrika.