Wednesday , 2nd Nov , 2016

Rapa mkali nchini Tanzania Nyandu Tozz amefunda ndoa mwishoni mwa wiki iliyopita na kutoa ya moyoni kuwa hata wagumu huwa nao wanaoa kwani mapenzi hayawezi kuzuilika na ndo maana hata wanajeshi hufikia wakati wakaoa.

Nyandu na Mkewe

 

Hata hivyo mwanadada aliyefunga ndoa na Nyandu hakuficha hisia zake na kumshukuru mme wake kuweza kudumu naye katika uchumba kwa miaka mitano na mwisho wa siku kumchangua yeye kuwa mke wake wa ndoa.

Pia Nyandu alitoa shukrani kwa wasanii wezake waliohudhuria katika harusi yake na kuwasihi mashabiki zake kwamba ndoa haitamrudisha nyuma kimuziki bali ataendelea na muziki na kuiwakilisha mitaa yake vizuri.