
Jux na Vanessa
Vanessa Mdee alisema haya kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV na kudai kuwa Jux kwenye suala la simu amekuwa mvivu sana na ndiyo jambo linaloleta tofauti kati yao.
"Mvivu wa simu amefarakanishwa na simu yake huyu jamaa, hata kwenye kujibu txt au kupokea simu hana ushirikiano na simu kabisaa kwa hiyo tunagombanaga mara nyingi kuhusiana na communication" alisema Vanessa Mdee