Tuesday , 19th May , 2015

Leo hii ikiwa ni siku 5 tu zimebakia kuelekea siku kubwa inayongojewa kwa hamu ya utoaji wa tuzo za filamu TAFA 2015, zoezi la kuwapigia kura washiriki na kazi zote za filamu zilizoingia katika kuwania tuzo hizo linaendelea kwa kasi.

Tuzo za filamu TAFA 2015

Namna ya kumpigia kura mshiriki unayempenda ni rahisi sana, andika code namba ya mshiriki unayempenda kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia simu yake na kuituma kwenda namba 15522.

Orodha nzima ya washiriki hao pamoja na kazi za filamu na code namba zake, kwa sasa inapatikana katika tovuti hii ambayo ni www.eatv.tv, na vilevile unaweza kuipata kupitia ukurasa wetu wa facebook.com/eatv.tv.

Kumbuka sherehe za ugawaji wa tuzo hizo zitafanyika tarehe 23 mwezi huu, katika ukumbi wa mikutano Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, piga kura mara nyingi uwezavyo kumuwezesha mshiriki unayempenda kuchukua tuzo.