Mimi Mars
Mars ambaye anafanya vizuri na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la 'Dedee' amesema kwa sasa yupo kwe wakati mgumu wa kujitofautisha na dada yake huyo kwai sauti zao zimekuwa zikiwachanganya mashabiki zao kiasi cha kuonekana kama Vanessa.
Akizungumza na eNewz ya EATV Mars amesema kwamba "Mission yangu ni kujitahidi kubadilisha suala la kufanana na Vanessa, kwani mashabiki na watu wengine wamekuwa wakisema tunafanana uimbaji . Nadhani kwa sababu bado ni mapema hawajazoea kwani mimi ni mgeni lakini niyahakikisha nakuwa tofauti ila ikishindikana kubadilika, nadhani watakuwa wameshazoea na hata kututofautisha wao wenyewe. Lakini niwe mkweli Vanessa siwezi kufanya naye kazi sahivi mpaka watu waweze kututofautisha ili isije ikaonekana yeye ndo kaimba wimbo wote peke yake, pia hatuwezi kuunda kundi moja la muziki bali tutaendelea kusaidiana na kuachia kazi huko mbeleni"- Mimi Mars.

Mimi Mars kushoto akiwa na dada yake Vanessa
Mtazame hapa Mars akiendelea kuifunguka mambo mengi zaidi.




