Friday , 5th Aug , 2016

Jaji wa shindano la kuibua vipaji vya uchezaji nchini maarufu kama Dance100% linaloendeshwa na EATV, Khalila amewataka washiriki waliofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kutobweteka badala yake waongeze juhudi ili waibuke washindi.

Jaji wa Dance100% Khalila

Akizungumza wakati wa majaji kugawana makundi kwa ajili ya mafunzo na mbinu mbalimbali za uchezaji, Jaji huyo amewataka kutambua kwamba kinachotafutwa ni ushindi ambao hautapatana kwa wao kuwa lelemama badi kufanya mazoezi kwa hari na morali ya hali ya juu.

‘’ Haya ni mashindano hivyo mshindi ni lazima apatikane, mmefanikiwa kupita hatua hii mnatakiwa kuthamini sana mazoezi pamoja na kuonyesha uwezo wa hali ya juu na hata mkiwafanikiwa kupita hatua moja inayofuata ndiyo muoneze juhudi zaidi ili muweze kutambulika ndani ya jamii na kuibuka na ushindi’’ Amesema Jaji Khalila.

Kwa upande wa Jaji mkongwe wa shindano hilo Super Nyamwela amewataka washiriki kuwa na nidhamu kuanzia mavazi hadi nishamu ya kuheshimu muda ili waweze kufikia malengo.

Aidha Jaji wa tatu wa shindano hilo Lotus amewataka washiriki wa shindano kutambua kwamba uchezaji ni ajira hivyo wajitume zaidi ili jamii iweze kuwapokea na kutumia vipaji vyao katika kupata burudani na vivyohivyo kujipatia kipato.

Shindano la Dance100% linarushwa na EATV pekee kila siku ya Jumapili kuanzia saa moja kamili jioni ambapo matukio yote yataonekana .

Tags: