Muigizaji Mboto aliyevaa jezi ya njano
Mboto ambaye mara kwa mara amekua akionekana kuikejeli Simba katika mitandao ya kijamii amesema wao ndiyo mabingwa wa kihistoria wa ligi na hata wakianza kwa kutoa sare huwa wanamaliza ligi kwa ubingwa kama walivyofanya msimu uliopita.
Amesema kwamba msimu uliopita Azam Fc walitwaa Ngao ya Jamii lakini mwishoni mwa msimu Yanga ikatwaa ubingwa,lakini msimu huu Simba wametwaa Ngao ya Jamii vivyo hivyo lazima ubingwa utatua kwao ukiwa ni wa msimu wa nne mfululizo.
Aidha ameenda mbali zaidi kwa kusema kwamba wao kama Yanga hawataki kuwa kama Rais wa Burundi Piere Nkurunziza hivyo pindi watakapotwaa ubingwa msimu huu watakaa chini na wanachama wenzao ili kuamua kuwaachia wapinzani wao ili wapate nafuu ya kuchekwa mitaani.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa VPL walianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Lipuli FC ya mkoani Iringa huku Simba ikiiunguruma kwa ushindi wa jumla ya bao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting na sasa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
Msikilize Mboto hapa chini,



