Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wanafunzi waomba mikopo itolewe kwa wote

Thursday , 18th Oct , 2018

Baada ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuweka wazi kuwa wanafunzi wenye vigezo wapatao elfu arobaini (40,000), ndio watapata mkopo kwa mwaka wa masomo 2018/19, Mtandao Wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) wasema idadi hiyo ni ndogo.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)

Akiongea leo kwenye MJADALA wa East Africa Television, Katibu wa Mtandao Wa Wanafunzi Tanzania, Joseph Malekela ameiomba bodi hiyo kuondoa ukomo wa idadi ya wanafunzi kwani sharti hilo linasababisha wanafunzi wengi kukosa elimu ya juu licha ya kuwa na vigezo vyote.

''Hii idadi ni ndogo sana ukilinganisha na wanafunzi waliofaulu kidato cha sita na wanahitaji mkopo, ni sawa na ilivyokuwa mwaka jana ambapo wanafunzi elfu thelathini pekee tu ndio walipata mkopo na kuacha waombaji wengi wakibaki nyumbani'', amesema Malekela.

Malekela amependekeza kuwa kwasababu mkopo huo ni deni na watu wanarudisha inabidi wote wapewe mkopo na sio kuwa na ukomo wa idadi kwa sababu ya sifa zilizowekwa ambazo kuna muda hazina uzito sana kwani kila anayeomba mkopo ana uhitaji.

Hata hivyo Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bodi ya mikopo Veneranda Malima, ambaye naye alikuwepo kwenye MJADALA amesema, lazima kuwepo na vigezo ambavyo vinawawezesha kutambua nani apate mkopo  na pia lazima viwepo vipaumbele ikiwemo Yatima na wasiojiweza.

Aidha Bi. Veneranda amefafanua kuwa ni ngumu kutoa mkopo kwa wanafunzi wote huku akibainisha kuwa wanafunzi waliokosa mkopo mwaka jana wameomba na wengine wamepata.
 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya