
Mshambuliaji wa Mbeya City, Eliud Ambokile
Akizungumza na www.eatv.tv, Ambokile amesema kuwa bado hajamalizana na Yanga na hana taarifa yoyote kama Yanga wameshafanya mazungumzo na klabu yake ya Mbeya City.
"Hapana, sio kweli sijamalizana na Yanga na sijajua kama wameshaenda Mbeya. Walinipigia tuu simu nikawaambia kuwa wafuate uongozi wangu," amesema.
Ambokile hivi sasa yuko katika kambi ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 ambayo inatarajia kucheza na timu ya taifa ya vijana ya Burundi katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya AFCON, mchezo ambao utachezwa usiku wa leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.