Wednesday , 8th Apr , 2015

Shirikisho la Ngumi Nchini BFT limesema hivi sasa linaendelea na mchakato wa kuunda timu ya Taifa ya Ngumi ya wanawake kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga amesema uundwaji wa timu hiyo ni maelekezo kutoka Chama cha Ngumi cha Dunia AIBA ambapo mwishoni mwa wiki hii watatangaza kikosi kizima cha Timu ya Taifa ambacho kitaanza mazoezi pamoja na timu ya Taifa ya wanaume.

Mashaga amesema, kambi hiyo itakuwa ni ya muda mrefu ili kuweza kuwajenga katika mchezo wa ngumi vijana hao ili kuweza kushiriki mashindano makubwa zaidi.