Bondia wa Martha George (aliyevaa red) akimsukumizia konde Irene Kimaro (aliyevaa bluu) kwenye mashindano ya ngumi za ridhaa ya Taifa yaliyokuwa yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania,BFT limepokea medali 300 za dhahabu, Shaba na Fedha kutoka shirikisho la masumbwi la Finland ikiwa ni sehemu ya msaada wa kuinua mchezo wa Ngumi nchini Tanzania.
Akiongea wakati akitoa msaada huo,kutoka Taasis ya michezo ya nchini Finland,Ari Kiovu anasema wameamua kutoa msaada huo ili kulipa fursa shirikisho la Masumbwi kuwekeza zaidi katika vifaa vya mchezo huo.
Kwa upande wake katibu wa BFT, Makore Mashaga amesema medali hizo watazitumia katika kuinua hamasa ya mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuandaa mashindano yatakayopelekea kuwapata mabondia watakaoweza kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kimataifa.