
Mashindano maalumu ya soka kwa mashabiki wa timu ya Barcelona yajulikanayo kama "Castle Lager Parfect Six" yanataraji kuanza May 24 mwaka huu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.
Meneja wa chapa Castle Lager Kabula Nshimo amesema ni fursa sasa kwa mashabiki kujikusanya na kuunda timu za wachezaji sita-sita kwaajili ya kushiriki ligi hiyo ambayo itaendeshwa kwa mtindo wa bonanza ambapo baadae timu iliyoshinda itakwenda nchini Hispania kwenda kuangalia live moja ya mechi za ligi kuu ya Hispania La Liga inayoihusisha timu ya FC Barcelona.