Monday , 10th Oct , 2016

Bondia Mtanzania Ibrahim Class anatarajia kupanda ulingoni Oktoba 28 mwaka huu kupambana na bondia kutoka Afrika Kusini Jason Bedeman katika Uzito wa Kilo 63 Ubingwa wa WBF.

Bondia Ibrahim Class

Muandaaji wa pambano hilo Jay Msangi amesema mpambano huo utatanguliwa na pambano kati ya Mtanzania Dullah Mbabe akipambana na Chengbo Zheng kutoka China katika uzito wa kilo 81 huku akiongeza kuwa mapambano hayo ambayo ni makubwa ya kimataifa yatasaidia mabondia hao kuwa katika maandalizi mazuri na ya mapema kwa ajili ya kuelekea katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2020.

Msangi amesema, kwa sasa wanahitaji kuwa na maandalizi ya mapema kwa mabondia kwa ajili ya kuwawezesha kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali hususani yaliyo mbele yao kwa sasa ya Olimpiki.