Monday , 22nd Feb , 2016

Michuano ya kombe la FA iliendelea tena usiku wa jana kwa michezo mitatu, Chelsea wakicheza uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge walifanikiwa kuwachapa Manchester city mabao 5-1.

Nyota wa Chelsea Eden Hazard (kushoto)akijaribu kumpita Fernando wa Manchester City.

Magoli ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na wachezaji Diego Costa, Willian borges, Gary Cahill, Eden Hazard, na bao la tano lilifungwa na Bertrand Traore dakika ya 89 ya mchezo huku bao la Manchester City likifungwa na mchezaji David Faupala.

Katika michezo mingine Blackburn Rovers ilichapwa na West Ham bao 5-1 , huku Tottenham Hotspurs wakifungwa na Crystal Palace bao 1-0.

Kwa matokeo hayo sasa Chelsea itamenyana na Everton katika mchezo wa Robo Fainali, Crystal Palace watasafiri kuikabili Reading, Watford watakuwa wageni kati ya Arsenal au Hull City na West Ham United itasafiri kuifuata Shrewsbury Town au Manchester United.

Arsenal watarudiana na Hull City kusaka hatua ya Robo Fainali, baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Emirates juzi, wakati Shrewsbury Town wataikaribisha Manchester United Jumatatu uwanja wa New Meadow kuanzia Saa 4:45 usiku.

Mechi hizo za Robo Fainali zitachezwa wikiendi ya Machi 11 na 14 mwaka huu.