Wednesday , 29th Apr , 2015

Chama cha mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam, DAREVA kimesema, kimeandaa mpango maalumu kwa waamuzi waliosomea ili kuhakikisha wanatumia elimu waliyoipata.

Akizungumza na East Africa Radio, mkufunzi kozi ya waamuzi DAREVA, Fredy Mshangama amesema, wameandaa ratiba maalumu ambapo kuna idadi ya mechi walizowekewa kuchezesha ambapo baada ya hapo atakuwa na utambulisho wa kuweza kuchezesha michezo mbalimbali.

Mshangama amesema, wamepanga kwa kila muamuzi kuchezesha mechi sita ambapo baada ya hapo atakuwa na uzoefu utakaomsaidia kuweza kushiriki mashindano yatakayoweza kumtambulisha katika ngazi za juu katika mchezo huo.