Friday , 30th Nov , 2018

Kiungo wa Simba Hassan Dilunga amesema kitendo chake cha kubaki uwanjani na mchezaji Ibrahim Job wa Lipuli wakati wa mapumziko kwenye mchezo wa ligi kuu, ni cha kawaida wala hakina uhusiano na imani za kishirikiana kama inavyodaiwa.

Hassan Dilunga akiwa na wachezaji wa timu pinzani.

Dilunga ametoa ufafanuzi huo akidai kuwa amewaacha watu wasema wanavyojisikia lakini yeye na Ibrahim Job walikuwa wanachezeana akili tu na ni mbinu tu za kulaghai wapinzani kwenye mchezo.

''Mimi nilikuwa nafanya utani tu siku ile lakini tukio zima halikuwa na maana yoyote, nilimsubiri Ibrahim Job atoke na mimi ndio nitoke na yeye akawa ananisubiri mimi ila siwezi kuzuia watu kusema wanachofikiria nafumba macho tu maisha yanaendelea'', amesema Dilunga.

Tukio la wawili hao kutegeana kutoka uwanjani wakati wa mapumziko, lilitokea uwanja wa taifa Ijumaa Novemba 23, 2018 ambapo mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya kutofungana.