
Wachezaji wa Liverpool
Mwana FA haamini kama Liverpool ambayo inaongoza ligi kuu ya EPL ikiwa na alama 51, kwenye mechi 19, itatwaa ubingwa wa msimu huu badala yake itakuwa kama mwaka 2013 ambapo pia waliongoza kwa muda mrefu na kushindwa kuchukua ubingwa.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Mwana FA ameweka ujumbe ulioambatana na picha ya nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard alipoteleza kwenye mechi dhidi ya Chelsea na kuifanya timu yake ifungwe na kupoteza mwelekeo kwenye mbio za ubingwa.
Watateleza tu..sina wasiwasi pic.twitter.com/MzXNldySz2
— ChoirMaster... (@MwanaFA) December 27, 2018
Katika misimu 10 iliyopita Liverpool ndio timu pekee ambayo iliongoza ligi kuu ya England mpaka wakati wa Krismasi na mwaka mpya lakini haikuchukua ubingwa huku timu zote zilizofanya hivyo ziliibuka mabingwa.
Liverpool iliongoza mwaka 2009 na kumaliza katika nafasi ya 2 nyuma ya Manchester United. Ikafanya hivyo tena mwaka 2013 na kumaliza katika nafasi ya 2.
Kwasasa Liverpool inaongoza ligi kwa tofauti ya alama 6 na timu ya Tottenham inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 45.