Thursday , 4th Feb , 2016

Mwanariadha Fabian Joseph ameanza kujipanga kusaka viwango vya kufuzu kucheza Olimpiki baada ya ushindi wake wa awali kuleta utata.

Fabian amesema, kwa sasa anakubaliana na shirikisho la Riadha Tanzania RT kuwa hajafuzu kucheza Olimpiki Rio 2016.

Fabiana amesema, ameamua kujipanga upya kwa kuwa Shirikisho nla Riadha la Dunia IAAF bado halijathibitisha kufuzu kwake.

Fabian amesema, awali alijua amefuzu baada ya kukimbia kwa saa 2:13:57 kumaliza mbio ya Kilomita 42 katika mashindano ya mwaliko kwa Niusu Marathon yaliyofanyika Desemba 20 mwaka jana nchini Japan.

Fabian amesema, tayari RT wameandika barua kwenda IAAF ili liweze kuthibitisha kama mashindano hayo yalitambuliwa au la lakini wakati akisubiri kupata majibu kutoka kwa IAAF ameanza kutafuta mashindano mengine ambayo yatamwezesha kupata viwango vya kufuzu kucheza Olimpiki mwaka huu.