Tuesday , 15th Apr , 2014

Chama cha mpira wa Magongo Dar es salaam kimeanza mchakato wa kusaka wachezaji wanawake wa mchezo wenye umri wa miaka 18 na 24 katika shule mbalimbali za sekondari wataoshiriki katika michuano ya awali ya mchujo wa kombe la Dunia.

Timu za Dar es salaaam zikichuana katika ligi ya Dar es salaam hivi karibuni

Chama cha mpira wa Magongo Dar es salaam kimeanza mchakato wa kusaka wachezaji wanawake wa mchezo wenye umri wa miaka 18 na 24 katika shule mbalimbali za sekondari wataoshiriki katika michuano ya awali ya mchujo wa kombe la Dunia inayotarajia kutimua vumbi June mwaka huu jijini Nairobi nchini Kenya.

Akiongea na EATV kwa njia ya simu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es salaamm, Mnonda Magani amesema kumekuwa na ushiriki hafifu wa wachezaji wanawake katika mchezo huo hali inayowalazimu kuwa na mpango maalum wa kuwapata wachezaji.

Magani amesema katika kufanikisha mpango huo wameanza na shule za Sekondari za Makongo na Shule ya kimataifa ya Tanganyika ambapo kwa upande wa wanaume watakaoshiriki michunao hiyo hawana wasiwasi kutokana na kuwa na timu nyingi za wanaume zilizoshiriki katika michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.