
Shomari Kapombe
Kapombe amesema kwa sasa anazidi kujiandaa vema kupitia mazoezi wanayopewa na benchi la ufundi la timu hiyo pamoja na mengine binafsi anayoyafanya peke yake.
“Mimi binafsi nimejiandaa vizuri na naendelea kujiandaa vizuri kwa mazoezi ambayo tunapewa na mengine ya kwangu binafsi, yote hayo nafanya ili kupambana na kurejesha makali yangu ili kuisaidia timu yangu," amesema Kapombe.
Kapombe amesema kwa sasa anaendelea vizuri na afya yake ipo vizuri kabisa kuweza kupambana kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara unaoanza Jumamosi ya wikiendi hii.
Kikosi cha Azam katika mazoezi
Azam FC inatarajia kufungua ng’we ya mzunguko wa pili kwa kushuka dimbani dhidi ya African Lyon Jumapili ya Desemba 18 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.