Bao alilofunga Didier Kavumbagu katika dakika ya 24 na kumuoingezea idadi ya magoli aliyofunga katika Msimu huu kuwa magoli 10 ni sawa na kisasi baada ya Azam Fc kufungwa bao 1-0 na Ndanda Fc mechi ya Mzunguko wa Kwanza, ambapo unaifanya Azam Fc kufikisha Pointi 33 baada ya kucheza mechi 17.
Kavumbagu Mshambuliahji wa Kimataifa wa Burundi alifunga bao hilo kwa mguu wa kulia akimalizia pasi ya Kipre Herman Tchetche na kuifanya Azam Fc kuwa kileleni mwa Ligi kuu Bara kwa Pointi 33.
Mabingwa hao watetezi, sasa wanaizidi Yanga Sc kwa Pointi mbili, ambayo hata hivyo mchezo mmoja mkononi, Jumatano ikitarajiwa kucheza na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.