Thursday , 24th Mar , 2016

Serikali,vyama vya michezo na kamati ya Olimpiki Tanzania TOC vikishirikiana kwa pamoja katika kuandaa timu, Tanzania inaweza kurudi na medali katika mashindano ya Olimpiki jijini Rio,mwezi Agosti mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania BMT Mohammed Kiganja ambapo amesema kama serikali kuna mambo wanayafanya kwa upande wao hasa katika kutafuta fedha,na hilo litafanikiwa kwa kuwa wamejipanga.

Kiganja amesema suala la kupeleka timu katika michuano ya olimpiki ni la pamoja,na akiachwa mtu mmoja, lengo halitofanikiwa.

Hadi sasa Tanzania,ina timu ya riadha pekee ambayo iko kambini, huku bado michezo mingine inatafuta wachezaji wa kufuzu mashindano hayo makubwa ya michezo duniani.