
Kikosi cha timu ya taifa ya vijana U13 na baadhi ya viongozi wakiwa Uwanja wa Amaan Zanzibar
Akizungumza na Hotmix Michezo Kocha Mirambo amesema, ziara katika mikoa mbalimbali zitasaidia kupata vijana wengine wenye uwezo zaidi ya walionao sasa na kuweza kufikia idadi wanayoihitaji ndani ya timu hiyo.
Mirambo amesema kwa sasa ana vijana 22 na lengo ni kuwa na vijana 35 ambao anaamini watakuwa na uwezo wa kuweza kufanya vizuri ndani ya timu.
Amesema, katika mkoa wa Morogoro waliweza kucheza mechi moja ambayo ilikuwa ni kipimo kizuri kwa vijana wake huku mechi ya Zanzibar akishindwa kupata vipaji vipya kutokana na jinsi mchezo ulivyokuwa kwani walicheza michezo miwili ambapo mchezo wa kwanza vijana wake waliweza kuibuka na ushindi wa bao 10-0 huku mchezo wa pili wakiibuka na ushindi wa bao 16-10.
Mirambo amesema, kwa sasa anaangalia zaidi mikoa ambayo wamelenga kufanya ziara kwa ajili ya kuweza kupata vijana wengine pamoja na mechi za kirafiki za kimataifa ambazo zitaweza kuwaweka fiti zaidi vijana wake.