
Jurgen Klopp
Klopp, amesema mchezo na Chelsea, ni nafasi nyingine muhimu, ya kurejesha matumaini ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu, lakini si kuwa mabingwa wa EPL, kwa sababu Chelsea, hawatapoteza mechi zote.
Endapo Liverpool, itapoteza mchezo wa leo, dhidi ya Chelsea, hiyo itakuwa ni mara ya nne kupoteza mechi kwenye uwanja wa nyumbani kwenye msimu huu.
Liverpool ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Chelsea kwenye msimu huu, lakini timu hizo zinakutana tena leo, kwenye mechi ya mzunguuko wa pili, zikiwa zinatofutiana kwa pointi 10.
Michezo mingine ya leo, ni pamoja, AFC Bournemouth na Crystal Palace, wakati Arsenal watawakiribisha Watford, uwanja wa Emirates.
Burnley itakuwa mwenyeji wa Leicester City, ambao wapo nafasi ya 15, ilhali Middlesbrough wakiikaribisha West Bromwich Albion, wakati Sunderland inayoshika mkia itakuwa na kazi ngumu dhidi ya Tottenham Hotspur, na Swansea City, wataoneshana kazi na Southampton.