Monday , 19th Nov , 2018

Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri, amesema kuwa mchanganyiko kati yake  na bosi wa Liverpool, Jurgen Klopp, kulimsaidia kutambua kwamba "amefikia kiwango cha juu" baada ya kuhama kutoka ligi kuu ya Italia 'Serie A' hadi ligi kuu nchini Ungereza, EPL.

Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri (kushoto) na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp (kulia)

Sarri amekuwa na mwanzo mzuri wa maisha katika EPL baada ya michezo 12 aliyosimamia katika klabu ya Chelsea mpaka sasa, akiweka rekodi mpya ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi akiwa na klabu hiyo, akionekana kufurahia sana uzoefu wake wa soka la Kiingereza baada ya kuondoka Napoli.

Chelsea na Liverpool walikutana katika mechi mbili mnamo mwezi Septemba, ambapo Maurizio Sarri amefichua siri juu ya mazungumzo yake nyakati tofauti tofauti na Klopp kwenye kingo zao za kusimama uwanjani.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 amekaririwa katika mahojiano na Gazzetta dello Sport, akisema: "Wakati fulani nikamgeukia na nikaona kwamba alikuwa ana furaha sanaNilikaribia nikamuuliza kwa nini."

"Aliniambia 'Mimi nina wakati mzuri, wewe?'. Mimi pia, 'nikamjibu.

"Hapa, unapoishi katika nyakati nzuri kama hizi, unatambua kuwa umefikia juu."

Pia kocha huyo wa Chelsea amemtaja Klopp kama kocha ambaye anavutiwa naye katika EPL kutokana na namna yake ya ufundishaji.

"Ninahisi kuwa karibu na Klopp kutokana na mtazamo wa falsafa zake, hata namna ya mazungumzo yetu yanavyokuwa ni katika hali bora sana," amesema Sarri. 

Chelsea na Liverpool zinakaribiana katika msimamo wa EPL mpaka sasa, Liverpool ikiwa katika nafasi ya pili kwa alama 30 huku Chelsea ikiwa katika nafasi ya tatu kwa alama zake 20 baada ya michezo 12.