Friday , 23rd Mar , 2018

Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza viingilio vya mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA kwa mwezi Machi kati ya Taifa Stars dhidi ya DR Congo ambapo moja ya viingilio vya chini ni shilingi 1,000.

Akiongea leo mbele ya wandishi wa habari msemaji wa TFF Clifford Ndimbo amesema mashabiki wa soka wataingia kwa shilingi 1,000 kwenye eneo la mzunguko ikiwa ni lengo la TFF kuwawezesha mashabiki wake kuona mchezo huo.

Viingilio vingine katika mchezo utakaopigwa Machi 27 ni ni Sh. 5,000 kwa majukwaa ya VIP A, B na C na mchezo huo utaanza Saa 10:00 jioni.

Tayari Taifa Stars ambayo inafundishwa na Salum Mayanga, imecheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki siku ya jana ambapo ilikubali kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa wenyeji Algeria.