Monday , 24th Mar , 2014

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya ngumi za ridhaa ya Tanzania Hassan Mzonge amesema kuwa amefurahishwa ni vipaji vya mabondia chipukizi walioongezwa katika timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya jumuiya ya madola itakayofanyika jijini Grascow

Aidha Mzonge amesema kuwa kwa sasa anawapa mazoezi ya stamina ya miguu na mikono zaidi baada ya kugundua mapungufu kwa vijana hao ambao wengi ndio kwanza wanachipukia katika mchezo huo

Mzonge ameongeza kuwa pamoja na vijana hao kujituma lakini bado wanachangamoto kubwa ya upungufu wa vifaa na hivyo amewaomba wadau kuisasidia timu hiyo ili iweze kujiandaa vizuri zaidi.