
Ibrahim Ajib akiwa anakokota mpira mbele ya wenzake.
Manara amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya mchezaji huyo kuonekana siku ya jana nje ya viwanja vya Taifa akiwa amepiga picha na shabiki wa Simba bila ya kuhofia jambo lolote lile.
"Najua nini una-miss dogo ila kafanye kazi hapa ni 'home anytime' umeondoka bila ya maneno ya hovyo, umetuheshimu na sisi tutakupa heshma yako", ameandika Manara.
Afisa habari wa Klabu ya Simba Haji Manara.
Kwa upande mwingine, Manara amemuhakikishia Ajib kuwa hatokuja kuona anasumbuliwa na shabiki yoyote kutoka katika timu hiyo kwa madai wafuasi wa Simba wamejawa na ustaarabu ndani ya nyoyo zao.
Ajib kwa sasa anachezea klabu ya Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo amesajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili katika dirisha la usajili wa msimu mpya wa Ligi 2017/2018.