
Kocha wa Biashara United Amri Said
Ushindi huo ni wa kwanza kwa Biashara kushinda kwenye wake wa nyumbani katika uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani humo.
Mabao ya Biashara yamefungwa na Daniel Manyenye dakika ya 18 na Juma Mpakala dakika ya 20, wakati bao la Mbeya City likifungwa na Frank Ikobela dakika ya 26.
Biashara United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, imejivuta kutoka mkiani baada ya kufikisha alama 13 katika mechi 18 na kuiacha Tanzania Prisons katika nafasi ya 20.