
Wachezaji wa timu za Coastal Union (nyekundu) na KMC (nyeupe) wakiomboleza kwa dakika 1 kabla ya mechi kuanza.
Misiba hiyo ni ule wa baba mzazi wa mshambuliaji wa Coastal Union Alikiba ambaye amefariki leo asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Msiba mwingine ni ule wa mchezaji wa zamani wa Taifa Stars, Hassan Gobos ambaye naye amefariki leo Januari 17, 2019.
Rais wa TFF Wallace Karia ametoa pole kwa familia ya Gobos pamoja na ndugu jamaa na wanafamilia wote wa mpira wa miguu nchini.
Aidha ameeleza kupokea kwa masikito taarifa za msiba huo kutokana na mchango mkubwa alioutoa marehemu Gobos enzi za uhai wake katika kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania.
Familia ya mpira jana pia ilimpoteza mdau mwingine Hamidu Mbwezeleni ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya TFF.